NAHODHA wa Chelsea, John Terry amekiri kuwa bado hajafanya mazungumzo yeyote na klabu hiyo kuhusu mkataba mpya lakini ana uhakika kuwa anaweza kuendelea kuitumikia katika msimu ujao wa Ligi Kuu. Terry mwenye umri wa miaka 34 amekuwa nguzo muhimu katika safu ya ulinzi ya kikosi cha Jose Mourinho msimu huu akiwa amecheza pia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain waliotoka sare ya bao 1-1 Juzi. Mkataba wa sasa wa Terry unamalizika mwishoni mwa mwezi Juni na kutokana na kuachiwa kuondoka kwa wakongwe wengine akiwemo Frank Lampard na Ashley Cole msimu uliopita kuna uwezekano pia Terry nao akaondoka. Akihojiwa Terry amesema klabu hiyo inajua nafasi yake pamoja na kutozungumza chochote kwani anajua kuna wachezaji wengine muhimu ambao wanatakiwa kubaki kuliko yeye.
No comments:
Post a Comment