Monday, March 30, 2015

AL SADD WAZIDI KUMKOMALIA XAVI.

MKURUGENZI wa michezo wa klabu ya Al Sadd, Mohammed Al Ali anaamini ujio wa Xavi unaweza kuisaidia timu hiyo kuiga staili ya tiki-taka inayotumiwa sana na klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania. Kiungo huyo wa Barcelona alikuwa jijini Doha mwishoni mwa wiki iliyopita ili kujadili uwezekano wa kujiunga na klabu hiyo kutokana na mustakabali wake Camp Nou kutojulikana. Klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Qatar ina matumaini ya kumshawishi mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35 kujiunga nao. Akihojiwa Al Ali amesema wana matumaini nyota huyo atajiunga nao kwani wanataka aina ya mchezo unaotumiwa na Barcelona na Hispania maarufu kama tiki-taka kuingia katika soka la nchi yao.

No comments:

Post a Comment