Monday, March 30, 2015

BAYERN YATAMBA KUONYESHA JEURI YA FEDHA USAJILI WA KIANGAZI.

MJUMBE wa kamati ya utendaji ya Bayern Munich, Jan-Christian Dreesen amekiri klabu hiyo inaweza kutumia kitita cha euro milioni 100 kwa ajili ya usajiliwa wa wachezaji nyota. Mabingwa hao wa Bundesliga bado hawajafikia vilabu vikubwa katika La Liga na Ligi Kuu wakati linapofikia suala la kutumia fedha nyingie katika usajili kwani ujio wa Javi Martinez wa kitita cha euro milioni 40 mwaka 2012 ndio usajili wa fedha nyingi kuwahi kufanywa na Bayern. Hata hivyo, Dreesen amebainisha kuwa hivi sasa wanaweza kuchuana na vilabu kama Real Madrid, Barcelona na Manchester United kwa kutumia fedha nyingi katika usajili. Dreesen amesema tofauti na huko nyuma hivi sasa Bayern ina uwezo wa kutumia kitita cha euro milioni 100 kwa ajili ya kumsajili mchezaji mmoja nyota.

No comments:

Post a Comment