Monday, March 30, 2015

YAYA TOURE KUAMUA HATMA YAKE IVORY COAST WIKI HII.

KIUNGO mahiri wa klabu ya Manchester City, Yaya Toure amesema anatarajia kuamua kuhusu mustakabali wake wa kuitumikia timu yake ya taifa ya Ivory Coast wiki hii. Akiwa nahodha Toure ameiongoza Ivory Coast kunyakuwa taji lao la kwanza la michuano ya Mataifa ya Afrika nchini Guinea Ikweta mapema mwaka huu toka wafanye hivyo tena mwaka 1992. Toure mwenye umri wa miaka 31 amesema anafikiria kufuata nyayo za kaka yake Kolo ambaye tayari amestaafu soka la kimataifa baada ya michuano hiyo. Akihojiwa Toure amesema anadhani malengo yake yametimia hivyo anataka kusubiri kwa siku chache kabla ya kuamua mustakabali wake. Nyota huyo anadhani wakati wake wa kuachia vijana chipukizi ili aweze kutilia mkazo klabu yake umefika.

No comments:

Post a Comment