Thursday, March 26, 2015

BENDTNER ATAMBA BAADA YA KUPIGA HAT-TRIC WAKATI DENMARK IKIISAMBARATISHA MAREKANI.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Denmark, Nicklas Bendtner amefurahia kiwango alichokionyesha wakati nchi yake ilipoitandika Marekani kwa mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa jana lakini anaamini angeweza kufunga mabao zaidi. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye ameanza kwa kusuasua katika klabu yake mpya ya Wolfsburg jana aliibuka nyota wa mchezo baada ya kufunga mabao mawili katika dakika za mwishoni na kuipa ushindi huo muhimu Denmark. Akihojiwa Bendtner amesema anadhani alicheza vyema na kama ingekuwa siku nyingine angeweza kufunga mabao zaidi kutokana na nafasi alizopata. Nyota huyo pia alimpongeza kocha wao Morten Olsen mwenye umri wa miaka 65 ambaye naye alikubaliana na mshambuliaji huyo kuwa Denmark ilistahili kushinda kwa mabao mengi zaidi.

No comments:

Post a Comment