Thursday, March 26, 2015

KOMBE LA MFALME KUFANYIKA KATIKA UWANJA WA CAMP NOU.

MCHEZO wa fainali ya Kombe la Mfalme kati ya Athletic Bilbao na Barcelona unaotarajiwa kuchezwa Mei 30 mwaka huu, utafanyika katika Uwanja wa Camp Nou. Kwa kawaida fainali ya michuano hiyo hufanyika katika uwanja huru lakini kutokana na klabu ya Real Madrid kukataa kutumika kwa uwanja wake wa Santiago Bernabeu kuliamuliwa kupigwa kura katika mkutano na Shirikisho la Soka la Hispania. Hakuna timu yeyote iliyotumia katika uwanja wake katika mchezo wa fainali toka mwaka 2002 wakati Deportivo La Coruna walipoifunga Real Madrid katika uwanja wao. Katika mkutano huo viwanja vya Vicente Calderon wa Sevilla na Mestalla wa Valencia vyote vilikuwa vikitafuta nafasi ya kuandaa fainali hiyo lakini waliondolewa katika duru la kwanza la kura na kubaki na Camp Nou pamoja na Uwanja wa San Mames wa Bilbao. Ushindi katika mchezo huo utaifanya Barcelona kufikisha mataji 27 ya michuano hiyo, wakati Bilbao wao wako katika nafasi ya pili katika orodha kwa kufikisha mataji 23 kama wakishinda.

No comments:

Post a Comment