BEKI wa klabu ya Bayern Munich, Jerome Boateng amesema kikosi chao kitafanya kila wawezalo kuhakikisha wanatinga hatua ya fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuingia hatua ya robo fainali kwa kishindo. Mabingwa hao wa Ujerumani ambao katika mchezo wao wa kwanza waling’ang’aniwa sare ya bila ya kufungana huko Ukraine jana walicharuka katika mchezo wao wa marudiano na kuinyuka bila huruma Shakhtar Donetsk kwa mabao 7-0. Katika mchezo huo mabao ya Bayern yalifungwa na Thomas Muller aliyefunga mawili, Boateng, Franck Ribery, Holger Badstuber, Roberto Lewandowski na Mario Gotze. Akihojiwa mara baada ya mchezo Boateng amesema lengo lao kubwa na kufika hatua ya fainali ambayo mwaka huu itachezwa huko jijini Berlin. Boateng alikiri kuwa bado ni safari ndefu kufikia huko lakini kwa aina kikosi walichonacho anadhani jambo liko ndani ya uwezo wao. Ratiba ya michezo ya robo fainali inatarajiwa kupangwa huko jijini Nyon, Machi 20 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment