MSHAMBULIAJI wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG, Zlatan Ibrahimovic amesema wachezaji wa Chelsea walijifanya kama watoto wakati wa tukio ambalo lilipelekea kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Nyota huyo wa kimataifa wa Sweden alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea faulo Oscar katika dakika ya 31 ya mchezo lakini PSG walifanikiwa kuwang’oa Chelsea katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kutoka nao sare ya mabao 2-2. Ibrahimovic amesema wakati akipewa kadi nyekundu wachezaji wote wa Chelsea walikuja kumzunguka hivyo akaona kama amezungukwa na watoto wengi. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa alivyopata kadi hiyo ilimchanganya kwakuwa hakuitegemea hususani kwa muda ule lakini anashukuru wachezaji wenzake waliendelea kucheza bila kukata tamaa na mwisho matokeo yakawa upande wao.
No comments:
Post a Comment