MSHAMBULIAJI mkongwe wa kimataifa wa Uruguay, Diego Forlan ametangaza rasmi kustaafu soka la kimataifa. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35 ameichezea Uruguay mechi 112 na kuifungia mabao 36 huku akiwa ameiwakilisha nchi hiyo katika fainali tatu za Kombe la Dunia na kuisaidia kushinda taji la Copa Amerika mwaka 2011. Akihojiwa Forlan amesema uamuzi aliochukua ni mgumu lakini anadhani wakati wake wa kufanya hivyo umefika ili kupisha njia kwa vizazi chipukizi. Forlan ambaye kwasasa ancheza soka katika klabu ya Cerezo Osaka ya Japan aliendelea kudai kuwa imekuwa ni heshima kwake kuvaa jezi ya timu ya taifa na kupeperusha bendera ya nchi yake kwa kipindi chote.
No comments:
Post a Comment