Thursday, March 12, 2015

WACHEZAJI GHANA WATUHUMIWA KUCHEZA KAMARI TIMU ZAO ZISHINDWE.

CHAMA cha Soka cha Ghana-GFA kimetoa taarifa katika vyombo vya sheria kuhusu baadhi ya wachezaji wa Ligi Kuu kutuhumiwa kucheza kamari ili timu zao zipoteze mchezo. Rais wa GFA Kwesi Nyantakyi amesema tuhuma hizo ni hatari kwa maendeleo ya soka ya nchi hiyo. Wiki iliyopita kocha wa klabu ya BA United, Mohammed Gargo aliwatuhumu wachezaji wake kupoteza mchezo kwa makusudi wakati wakicheza na timu ya All Stars. Baadae ilikuja kuripotiwa kuwa kocha huyo alitimuliwa na klabu yake kutokana na kauli yake hiyo. Nyantakyi amesema wameshalifikisha jambo hilo kwa vyombo husika kwa ajili ya uchunguzi na yeyote atakayebainika kuhusika kwa namna moja au nyingine hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

No comments:

Post a Comment