Monday, March 30, 2015

CHELSEA WAMTENGEA BALE KITITA CHA PAUNDI MILIONI 75.

KLABU ya Chelsea inaripotiwa kuwa inajipanga kutenga kitita cha paundi milioni 75 kwa ajili ya kumng’oa winga wa Real Madrid Gareth Bale katika majira ya kiangazi. Chelsea wamekuwa wakihusishwa na taarifa za kumtaka Bale katika wiki chache zilizopita kufuatia tetesi kuwa nyota huyo anataka kuondoka Madrid. Na sasa taarifa zinadai kuwa Chelsea wako tayari kutoa kitita cha paundi milioni 75 kwa ajili ya kupata saini ya winga huyo wa kimataifa wa Wales. Bale bado anadai anafurahia kuendelea kuwepo Madrid lakini Chelsea wanajipanga kumpa ofa ya mshahara wa paundi 300,000 kwa wiki ili kukamilisha usajili wake. Kama akiamua kuondoka Madrid Bale ndio atakuwa mchezaji anayelipwa zaidi Chelsea.

No comments:

Post a Comment