Monday, March 30, 2015

WENGER AMVALIA MABOMU RAHEEM STERLING.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anajipanga kuingia katika kinyang’anyiro cha kutaka kumsajili winga wa Liverpool Raheem Sterling katika majira ya kiangazi. Wenger amekuwa akimhusudu sana nyota huyo na yuko tayari kujaribu bahati yake kutokana na sakata juu ya mkataba linaloendelea katika klabu yake. Sterling mwenye umri wa miaka 20 amesimamisha mazungumzo kuhusu mustakabali wake mpaka majira ya kiangazi ili kuhamishia nguvu zake katika soka lakini Liverpool wanahofu kuwa hatasaini mkataba mpya. Kuchelewa huko kumezigutusha klabu kubwa ambazo pia zinamtamani wakiwemo Real Madrid, Bayern Munich na Manchester City. Arsenal nao wanajipanga kuingia katika kinyang’anyiro hicho kujaribu tena kumsajili baada ya kushindwa kumsajili wakati akiwa na miaka 10 mwaka 2010.

No comments:

Post a Comment