Tuesday, March 31, 2015

FALCAO AFIKIA REKODI YA MABAO COLOMBIA.

MSHAMBULIAJI nyota anayekipiga kwa mkopo Manchester United, Radamel Falcao amefanikiwa kufikia rekodi ya mabao katika timu yake ya taifa ya Colombia baada ya kufikisha mabao 24 jana. Falcao alichukuliwa kwa mkopo kutokea AS Monaco, amefikia rekodi hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Arnoldo Iguaran baada ya kufunga bao kwa njia ya penati wakati Colombia ikiigaragaza Kuwait kwa mabao 3-1. Hilo linakuwa bado la tatu kufungwa na Falcao katika michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa aliyoichezea Colombia baada ya kufunga mengine mawili wakati waliposhinda mabao 6-0 dhidi ya Bahrain. Falcao mwenye umri wa miaka 29 amekuwa na msimu mbaya toka atue United kwani amefanikiwa kufunga mabao manne pekee katika michezo 22 aliyocheza msimu huu.

No comments:

Post a Comment