Tuesday, March 31, 2015

QATAR SASA MWENDO MDUNDO.

OFISA wa kamati ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar amesema hadhani kama kutahitajika vipoza hewa katika viwanja kama ilivyoahidiwa wakati wakitafuta nafasi hiyo. Mapema mwezi huu Shirikisho la Soka Duniani-FIFA lilitegua kitendawili cha muda mrefu wa muda gani haswa michuano hiyo itachezwa na kuamua kuwa ichezwe wakati wa majira ya baridi ya Novemba na Desemba mwaa huo. Changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakabili katika kuandaa michuano hiyo wakati wa kiangazi ilikuwa ni jinsi na kutengeneza vipoza hewa kwa ajili ya joto kali linafikia nyuzi joto 40 wakati huo. Hata hivyo sasa ofisa huyo Dario Cadavid amesema kuwatakuwa hakuna umuhimu tena wa kutumia vipoza hewa kwasababu michuano hiyo itafanyika wakati wa majira ya baridi kama ilivyoamuliwa. Pamoja na hayo Cadavid aliendelea kudai kuwa bado wataufanyia kazi mfumo huo wa vipoza hewa kwa ajili ya mechi zao chache za ligi ambazo huchezwa wakati wa joto kali.

No comments:

Post a Comment