Tuesday, March 31, 2015

UEFA YAZISHITAKI MONTENEGRO NA URUSI.

SHIRIKISHO la Soka Ulaya-UEFA limevishitaki vyama vya soka vya Montenegro na Urusi kufuatia mchezo baina ya timu zao za taifa wa kufuzu michuano ya Ulaya mwakani kushindwa kufanyika huko Podgorica. Mchezo huo ulisitishwa katika kipindi cha pili baada ya vurugu zilizowahusisha wachezaji na viongozi huku golikipa wa Urusi Igor Akinfeev akitolewa mapema kwa kupigwa fataki kutokea jukwaani. Montenegro wao wanashitakiwa kwa kuandaa mchezo ambao haukuchezwa ukamalizika wakati nchi zote mbili zikishitakiwa kwa mashabiki wake kurusha mafataki na vitu vingine uwanjani. Urusi wao wametuma malalamiko yao rasmi UEFA wakitaka kupewa ushindi wa mchezo huo ambao mpaka unasimamishwa na mwamuzi Diniz Aytekin hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.

No comments:

Post a Comment