Tuesday, March 31, 2015

XAVI AKANUSHA KUSAINI MKATABA AL SADD.

KIUNGO wa Barcelona Xavi Hermandez amekanusha taarifa kuwa anajipanga kusaini mkataba na klabu ya Al Sadd inayoshiriki Ligi Kuu nchini Qatar. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania alitumia siku nne za mapumziko kupisha michezo ya kimataifa nchini Qatar huku rais wa Al Sadd Mohammad Al Ali akidai kuwa na uhakika wa kumsajili mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35. Hata hivyo, baada ya kurejea Hispania, Xavi amesisitiza kuwa alienda Qatar kwa ajili ya mapumziko na familia yake na sio vinginevyo. Xavi anategemewa kwa kiasi kikubwa kuondoka Barcelona mwishoni mwa msimu huu baada ya kuitumikia kwa miaka 24 toka alipoibuka kutoka katika academy maarufu ya timu hiyo ya La Masia. Mbali na Al Sadd, Xavi pia amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda katika timu ya New York City FC ya Marekani ambako ataweza kukutana na mchezaji mwenzake wa zamani David Villa.

No comments:

Post a Comment