Tuesday, March 31, 2015

PSG YAWANIA KUNYAKUWA DI MARIA.

MATAJIRI wa Ufaransa klabu ya Paris Saint-Germain wako tayari kuwarudishia Manchester United fedha yao kwa ajili ya kumsajili Angel Di Maria. Di Maria mwenye umri wa miaka 27 amekuwa chini ya kiwango toka asajiliwe kwa kitita kilichovunja rekodi cha paundi milioni 59.7 kutoka Real Madrid kiangazi mwaka jana. PSG ambao pia walikuwa wakimtaka mwaka jana, wako tayari tena kutoa kitita kikubwa kwa ajili ya kumng’oa nyota huyo Old Trafford. Kitu kikubwa kinachowapa nafasi PSG kumchukua nyota huyo kiangazi ni uhakika wa ushiriki wao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ukilinganisha na United ambao bado wanapigana kupata nafasi hiyo. Tayari meneja wa United Louis van Gaal ameshamfungulia milango Di Maria kwa kukiri kuwa hatakuwa na mpango wa kumzuia kama akiamua kuondoka.

No comments:

Post a Comment