Wednesday, April 1, 2015

MADRID YAMNASA DANILO KUTOKA PORTO.

KLABU ya Real Madrid imefikia makubaliano na Porto kwa ajili ya kumnunua beki wa kimataifa wa Brazil Danilo na anatajiwa kujiunga na mabingwa hao wa Ulaya msimu ujao. Taarifa ya klabu hiyo iliyotumwa katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter iliongeza kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye hupendelea kucheza zaidi nafasi ya beki wa kulia amepewa mkataba wa miaka sita ambao utamalizika Juni 30 mwak 2021. Katika taarifa yake Porto imedai kuwa itamuuza beki huyo kwenda Madrid kwa kitita cha euro milioni 31.5. Danilo alianza soka lake katika klabu ya nchi kwake Brazil ya America kabla ya kujiunga na Santos na baadae kwenda Porto Januari mwaka 2012 ambako amefanikiwa kushinda mataji mawili ya ligi.

No comments:

Post a Comment