Wednesday, April 1, 2015

BLATTER KUHUDHURIA MKUTANO MKUTANO MKUU CAF.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter anatarajiwa kushiriki mkutano mkuu wa 37 wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF ambao utafanyika Aprili 7 mwaka huu jijini Cairo, Misri. Blatter ambaye anagombea kipindi cha tano kuongoza FIFA, anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo ukiwa umebaki mwezi mmoja kabla ya shirikisho hilo halijafanya uchaguzi mkuu wa rais. CAF tayari wameweka bayana msimamo wao kuwa watamuunga mkono Blatter katika uchaguzi huo ambao utamfanya kuwa rais wa tatu kulitumikia shirikisho hilo muda mrefu baada ya Jules Rimet na Joao Havalange kama akifanikiwa kushinda. Wiki iliyopita Blatter amesema hatahitaji kujinadi kama walivyo wapinzani wake kwani watu wote wanatambua kazi kubwa aliyofanya katika miaka 17 akiwa rais wa FIFA. Blatter atachuana na makamu wa rais wa FIFA na mwenyekiti wa Shirikisho la Soka la Jordan, Prince Ali Bin Al Hussein, mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Ureno, Luis Figo na rais wa Chama cha Soka cha Uholanzi Michael van Praag.

No comments:

Post a Comment