Wednesday, March 25, 2015

FALCAO A-BEEP KUONDOKA UNITED.

MSHAMBULIAJI wa Manchester United Radamel Falcao amedokeza jana kuwa anaweza kuondoka katika timu hiyo mwishoni mwa msimu kutafuta timu anayoweza kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara. Nyota huyo wa kimataifa wa Colombia alikosa michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana kutokana na majeruhi, baadae alihamia United kwa mkopo akitokea Monaco ya Ufaransa ambako ameshindwa kutamba. Akihojiwa Falcao amesema anafikiri kila mchezaji anahitaji kucheza na anafurahia kucheza ndio maana anataka kuisaidia United katika michezo nane ya Ligi Kuu iliyobakia na baada ya hapo chochote kinaweza kutokea. Falcao aliendelea kudai kuwa wakati msimu utakapokwisa atakaa chini na kufanya tathmini na kuamua kitu gani kitakuwa bora kwake. Nyota huyo amesema anahitaji kutafuta mahali ambapo anaweza kupata nafasi kucheza mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment