Wednesday, March 25, 2015

USHANGILIAJI KUMPONZA RONALDO.

RAIS wa Ligi ya Soka ya Hispania-LFP, Javier Tebas amedai kuwa mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anaweza kufungiwa kwa kosa la ushangiliaji wakati aliposawazisha bao katika mchezo wa Jumapili iliyopita dhidi ya Barcelona. Ronaldo sio mara yake ya kwanza wakati akifunga bao katika Uwanja wa Camp Nou kuonekana akiwataka mashabiki wa Barcelona kutulia kwani alifanya hivyo tena katika mchezo uliopita. Tebas amesema wanatakiwa kuwa waangalifu na ushangiliaji wa aina yeyote wenye ujumbe wa uchochezi wa mchezaji wakati akifunga bao au kwenye tukio lolote kwani kunaweza kuzuka vurugu zinazowea kusababisha maafa. Rais huyo aliendelea kudai kuwa suala hilo litaangaliwa kwa makini na kuna uwezekano Ronaldo akatozwa faini au hata kufungiwa.

No comments:

Post a Comment