Wednesday, March 25, 2015

JUVENTUS HAINA UBAVU WA KUMZUIA POGBA KUONDOKA - MAROTTA.

OFISA mkuu wa Juventus, Giuseppe Marotta hadhani kama klabu hiyo itaweza kumzuia kiungo Paul Pogba kama ataamua anataka kwenda kucheza mahali pengine katika majira ya kiangazi. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa kihusishwa na vilabu kadhaa tajiri katika miezi ya karibuni vikiwemo Real Madrid, Paris Saint Germain na Chelsea ana kumekuwa na tetesi kuwa anaweza kufikia thamani ya euro milioni 100. Ingawa Marotta amesisitiza kuwa mpaka sasa Pogba hajaonyesha nia yeyote ya kuondoka, anafikiri itakuwa jambo lisilowezekana kumbakisha Turin kama akiamua kutafuta changamoto nyingine. Marotta amesema Pogba mwenyewe ndio atakaeamua mustakabali wake wa aidha kubakia Italia au kwenda sehemu nyingine kwani hawataweza kushindana na vilabu tajiri wakiamua kumpa kitita kikubwa zaidi yao. Juventus inayonolewa na Massimiliano Allegri hivi sasa ipo kileleni mwa Serie A kwa tofauti ya alama 14.

No comments:

Post a Comment