Wednesday, March 25, 2015

PIQUE AWAPONDA WANAOMKOSOA CASILLAS.

BEKI wa klabu ya Barcelona, Gerard Pique anaamini golikipa Iker Casillas ndio angekuwa shujaa wake kama angekuwa mshabiki wa Real Madrid. Beki huyo mwenye umri wa miaka 28 amekuwa akicheza pamoja na Casillas katika timu ya taifa ya Hispania toka mwaka 2009 wakati alipoitwa kwa mara ya kwanza baada ya kurejea Barcelona akitokea Manchester United. Baada ya kuwa chini ya kiwango mwaka jana, Pique amerejea tena katika ubora wake mwaka huu na kuisaidia Barcelona kuwafunga mahasimu wao Madrid Jumapili iliyopita. Pique amewaponda wale wanaobeza uwezo Casillas kwani bado anaamini anaweza kurejea katika kiwango chake cha juu kabisa. Nyota huyo amesema kama angekuwa mshabiki wa Madrid, Casillas ndio angekuwa shujaa wake kwani ni mfano kwa wachezaji wote wa timu hiyo.

No comments:

Post a Comment