Tuesday, March 17, 2015

FIFA YAAMURU RAYON SPORTS KUKATWA ALAMA KWA KUMNYIMA SHUNGU HAKI YAKE.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limeiamuru Shirikisho la Soka la Rwanda-Ferwafa kuikata alama tatu katika ligi klabu ya Rayon Sports ikiwa ni moja ya adhabu waliyopewa kwa kushindwa kumlipa kocha wao wa zamani Raoul Shungu. Mapema mwezi huu, FIFA ilituma barua kuielekeza klabu hiyo kumlipa kocha huyo haraka kabla ya kuchukuliwa hatua kali. Shungu alikuwa akiidai Rayon kiasi cha dola 18,828 ikiwa ni sehemu ya malipo yake wakati akiinoa klabu hiyo mwaka 2008. Wakati huo inaripotiwa kuwa maofisa wa klabu hiyo walikubali kocha huyo kutumia fedha zake mwenyewe kwa ajili ya kuwasajili wachezaji kama Honore Kabongo, Bokota Labama, Jean Lomami na Jimmy Kidega. Shungu pia amesema alitumia fedha zake mwenyewe kununua baadhi ya vifaa kama mipira, neti na vifaa vingine vya mazoezi lakini hajarudishiwa fedha hizo toka wakati huo.

No comments:

Post a Comment