TIMU ya Taifa ya Wanawake-Twiga Stars inatarajiwa kuondoka nchini Ijumaa hii kuelekea Zambia kwa ajili ya mchezo wao wa mkondo wa kwanza dhidi ya nchi hiyo utakaofanyika Jumapili hii. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na Shirikisho la Soka nchini-TFF Twiga Stars inatarajiwa kuondoka na msafara wa watu 25 kwa ajili ya mchezo huo wa kuwania kufuzu michuano ya Afrika kwa Wanawake. Kama wakifanikiwa kuwaondoa Zambia, Twiga Stars itakuwa imefuzu moja kwa moja michuano hiyo. Wakati huohuo timu ya taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni nayo inatarajiwa kuondoka nchini Alhamisi hii kwa ajili ya mchezo mariadiano dhidi ya Misri utakaofanyika jijini Cairo. Tanzania ina kibarua kizito kushinda katika mchezo huo baada ya kufungwa ule wa kwanza kwa mabao 6-2, ili waweze kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika kwa soka la ufukweni itakayofanyika katika visiwa vya Shelisheli.
No comments:
Post a Comment