MENEJA wa klabu ya AC Milan, Filippo Inzaghi ana matumaini ya kuendelea na kibarua chake pamoja na kipigo cha mabao 2-1 walichopata kutoka Fiorentina. Kipigo hicho kinaifanya Milan kuzidi kudidimiza ndoto zao za kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao hivyo kuongeza msukumo juu ya mustakabali wa Inzaghi. Hata hivyo kocha huyo ameonyesha bado ana matumaini ya kuendelea na kibarua chake baada ya kudai kuwa bado ataendelea kuutumikia mkataba wake na timu hiyo. Inzaghi amesema anajua wanapitia katika kipindi kigumu lakini jambo la msingi ni kuhakikisha wanakuwa pamoja na kuendelea kucheza soka safi. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa ana matumaini ya kuendelea kuinoa Milan kwa kipindi kirefu kijacho kama watahitaji kumbakisha.
No comments:
Post a Comment