Tuesday, March 24, 2015

MADRID YAANZA KUWACHUKULIA HATUA MASHABIKI WALIOSHAMBULIA MAGARI YA WACHEZAJI.

KLABU ya Real Madrid imemsimamisha mjumbe mmoja wa timu hiyo na kuwabaini mashabiki wengine wawili waliohusika kubugudhi na kupiga magari ya baadhi ya wachezaji baada ya mchezo dhidi ya Barcelona. Mshabiki mmoja walinaswa katika picha za video akishambulia kioo cha gari la Jese na wengine wawili wakijaribu kulipiga mateke gari la Gareth Bale. Beki Sergio Ramos pia alikuwepo eneo hilo wakati tukio likitokea ambapo alisimamisha gari lake na kujaribu kuwaambia mashabiki hao kuwa wanachofanya sio sahihi. Bale alijiunga na Madrid akitokea Tottenham Hotspurs katika majira ya kiangazi mwaka 2013 na amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha timu hiyo kilichoshinda Kombe la Mfalme na taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita. Hata hivyo msimu huu umekuwa sio mzuri kwa Bale kwani amekuwa akiandamwa na majeruhi na kupelekea kutokuwa fiti kwa asilimia mia moja hivyo kuwafanya mashabiki kumzomea katika baadhi ya michezo.

No comments:

Post a Comment