Tuesday, March 24, 2015

SHABIKI WA LIVERPOOL AJINADI KUMZUIA BALOTELLI KUTOPATA KADI YA PILI YA NJANO.

SHABIKI mmoja wa Liverpool amedai kuwa yeye ndio aliyesaidia kuepusha kadi ya pili nyekundu katika mchezo wa Jumapili iliyopita dhidi ya Manchester United baada ya kumzuia Mario Balotelli kutokwenda kumvaa Chris Smalling. Wakiwa tayari wamempoteza nahodha wao Steven Gerrard aliyetolewa baada ya kucheza kwa sekunde 38 toka alipoingia kipindi cha pili, Liverpool tayari walikuwa na upungufu wakati Balotelli aliyekuwa na kadi ya njano alipotaka kukwaruzana na Smalling baada ya kukwatuliwa. Hatua hiyo ilimfanya Balotelli kupepesuka mpaka pembeni mwa uwanja sehemu za matangazo na shabiki huyo Shaun Leatherbarrow aliyekuwa karibu amesema ilikuwa ni jukumu lake kumtuliza mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Italia. Shabiki huyo amesema alifanya hivyo baada ya kuona jinsi Balotelli alivyochukizwa na kitendo hicho na pengine angeweza hata kumvaa Smalling kama asingemtuliza na kupata kadi nyingine ya njano.

No comments:

Post a Comment