Wednesday, March 25, 2015

MAJERUHI WAMPAGAWISHA HODGSON.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson anategemea wachezaji zaidi kujitoa katika kikosi chhake baada ya mchezo wao wa kufuzu michuano ya Ulaya mwaka 2016 dhidi ya Lithuania. Nyota wa Liverpool Daniel Sturridge na Adam Lallana wote waliondolewa katika kikosi cha timu hiyo juzi kutokana na majeruhi huku Luke Shaw na Fraser Forster nao wakitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita. Kutokana na hali jinsi ilivyo, Hodgson anaamini anaweza kuwapoteza wachezaji zaidi kwa majeruhi mara baada ya mchezo wao dhidi ya Lithuania. Wachezaji wengine wa timu hiyo kama Wayne Rooney, Raheem Sterling na Harry Kane wanaonekana kama hawako fiti kwa asilimia mia moja kwa mujibu wa kocha huyo.

No comments:

Post a Comment