Wednesday, March 25, 2015

SKRTEL AKANUSHA KUMKANYAGA DE GEA KWA MAKUSUDI LAKINI ASHINDWA RUFANI.

BEKI wa Liverpool, Martin Skrtel amekanusha mashitaka anayotuhumiwa kwa kumkanyaga golikipa wa Manchester United David De Gea. Tukio hilo lilitokea katika dakika za majeruhi ya mchezo kati ya timu hizo ambapo United iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika Uwanja wa Anfield Jumapili iliyopita. Beki huyo wa kimataifa wa Slovakia mwenye umri wa miaka 30, alishitakiwa jana na anakabiliwana adhabu ya kufungiwa mechi tatu lakini mwenyewe amedai tukio hilo lilikuwa bahati mbaya. Mwamuzi wa mchezo huo Martin Atkinson hakuliona tukio hilo lakini waamuzi watatu wa zamani wamekubaliana kuwa alitakiwa kutolewa nje baada ya kuona marudio ya picha za video. Kama Skrtel akifungiwa mechi hizo inamaanisha kuwa ataukosa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Arsenal utakaochezwa Aprili 4 mwaka huu na mwingine dhidi ya Newcastle United utakaochezwa Aprili 13 pamoja na ule wa maruadiano ya robo fainali wa Kombe la FA dhidi ya Blackburn Rover Aprili 8. Nahodha wa timu hiyo Steven Gerrard tayari atakosa michezo hiyo baada ya kunyukwa kadi nyekundu katika mchezo huo baada ya kupita sekunde 38 toka aingie akitokea benchi katika kipindi cha pili.

No comments:

Post a Comment