Wednesday, March 25, 2015

UINGEREZA KUTAFUTA UENYEJI WA KOMBE LA DUNIA 2026.

MWENYEKITI wa Chama cha Soka cha Uingereza-FA, Greg Dyke amesema nchi hiyo inaweza kufikiria kuingia katika kinyang’anyiro cha kutafuta uenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2026. Uingereza iliingia katika kinyang’anyiro cha kutafuta uenyeji wa fainali za mwaka 2018 lakini walishindwa vibaya na Urusi waliopewa jukumu hilo. Hata hivyo Dyke amesema jaribio lao litategemea kama rais wa sasa wa Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA Sepp Blatter ataendelea kubakia madarakani. Dyke aliendelea kudai kuwa pia kuteuliwa kwa David Gill raia wa Uingereza katika kamati kuu ya uongozi wa FIFA inaweza kuongeza ushawishi wa kugombea nafasi hiyo. Mwenyekiti huyo wa FA amesema Uingereza itachukua hatua hiyo iwapo tu sera zitakuwa za wazi lakini haitaomba nafasi hiyo wakati Blatter akiwa bado yuko madarakani.

No comments:

Post a Comment