KIUNGO wa klabu ya Juventus, Paul Pogba anatarajiwa kukosa mechi za robo fainali za michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupata majeraha ya msuli wa paja katika mchezo dhidi ya Borussia Dortmund. Pogba mwenye umri wa miaka 22 alitolewa nje katika kipindi cha kwanza katika ushindi wa mabao 3-0 waliopata Juventus juzi na sasa anatarajiwa kukaa nje kwa siku 50. Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United pia anatarajiwa kukosa michezo ya kirafiki ya kimataifa ya Ufaransa ambayo watacheza na Brazil na Denmark. Kama Pogba akirejea kama ilivyopangwa, ataweza kucheza mechi tatu za mwisho za ligi pamoja na mechi ya mkondo wa pili ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa kama Juventus watafanikiwa kufika huko. Juventus kwasasa wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama 14 hivyo kuwaweka katika nafasi nzuri ya kunyakuwa taji hilo kwa mara ya nne mfululizo.
Friday, March 20, 2015
PIGO JUVENTUS: POGBA KUKOSA ROBO FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA.
KIUNGO wa klabu ya Juventus, Paul Pogba anatarajiwa kukosa mechi za robo fainali za michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupata majeraha ya msuli wa paja katika mchezo dhidi ya Borussia Dortmund. Pogba mwenye umri wa miaka 22 alitolewa nje katika kipindi cha kwanza katika ushindi wa mabao 3-0 waliopata Juventus juzi na sasa anatarajiwa kukaa nje kwa siku 50. Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United pia anatarajiwa kukosa michezo ya kirafiki ya kimataifa ya Ufaransa ambayo watacheza na Brazil na Denmark. Kama Pogba akirejea kama ilivyopangwa, ataweza kucheza mechi tatu za mwisho za ligi pamoja na mechi ya mkondo wa pili ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa kama Juventus watafanikiwa kufika huko. Juventus kwasasa wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama 14 hivyo kuwaweka katika nafasi nzuri ya kunyakuwa taji hilo kwa mara ya nne mfululizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment