KIUNGO mahiri wa Juventus, Paul Pogba amekielezea kitita cha euro milioni 200 kwa ajili ya usajili wake kuwa ni jambo la kuumiza kichwa wakati tetesi za usajili juu yake zikizidi kuendelea. Wakala wa nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa anadaiwa kuiambia Barcelona kuwa wanapaswa kulipa kitita cha euro milioni 200 kwa kujumuisha ada na mshahara wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 Januari mwakani. Ingawa Pogba amesaini mkataba mpya na Juventus mwaka jana lakini taarifa za kuondoka kwake zimekuwa zikivuma toka Januari mwaka huu huku Real Madrid na Chelsea zikitajwa kumuwinda katika majira ya kiangazi. Pamoja na hayo Pogba mwenyewe amesema hataki kuumiza kichwa kuhusu masuala hayo kwnai jambo analotaka ni kuzingatia kiwango chake na kujaribu kuisaidia Juventus kushinda mataji. Pogba amesema mambo yake kuhusu usajili amemuachia wakala wake Mino Raiola kushughulika nayo hivyo yeye kwasasa hajui lolote linaloendelea.
No comments:
Post a Comment