POLISI WACHUNGUZA TWITTER ZA KIBAGUZI KUMUENDEA WELBECK.
POLISI katika mji wa Manchester wamesema wanafahamu kusuhu ujumbe wa kibaguzi katika mtandao wa kijamii wa twitter kumuendea mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck. Ujumbe ulikuja kufuatia Welbeck kufunga bao la ushindi la Arsenal dhidi ya klabu yake ya zamani ya Manchester United katika robo fainali ya Kombe la FA Jumatatu iliyopita. Vita vya ubaguzi Ulaya bado inaonekana kuwa ngumu kufuatia matukio kama hayo kuzidi kuongezeka siku hadi siku, hivi karibuni mashabiki wa Chelsea walinaswa katika picha za video wakimzuia mtu mweusi kuingia katika treni jijini Paris. Chelsea tayari imeshawasimamisha mashabiki watano kuhusiana na tukio hilo ambalo lilitokea kabla ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya timu hiyo na Paris Saint Germain.
No comments:
Post a Comment