MENEJA wa klabu ya Zenit Saint Petersburg Andre Villas-Boas ameomba radhi kwa utata uliojitokeza kati yake na benchi la ufundi la timu ya Torino baada ya kikosi chake kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa League jana. Zenit walitinga hatua hiyo kwa mara ya kwanza toka mwaka 2008, mwaka ambao ndio walishinda Kombe la UEFA, pamoja na kufungwa bao 1-0 na Torino katika mchezo wao huo wa marudiano. Ushindi wa mabao 2-0 waliopata nyumbani dhidi ya Torino katika mchezo wao wa mkondo wa kwanza uliwasaidia Zenit kutinga hatua hiyo kwa jumla ya mabao 2-1. Pamoja na kuvuka, Villas-Boas ambaye amewahi kuzinoa Chelsea na Tottenham Hotspurs aliingia katika mzozo na kujibizana maneno makali na benchi la ufundi la Torino hatua ambayo imepelekea kuomba radhi. Akihojiwa Villas-Boas alikiri kufanya kosa kwa tabia aliyoionyesha na kuomba radhi kwani akiwa kama kocha hakupaswa kushindw akudhibiti hasira zake.
No comments:
Post a Comment