Tuesday, March 17, 2015

WAZIRI MKUU WA UFARANSA AMSHANGAA IBRAHIMOVIC.

WAZIRI mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls amekiri kushtushwa na kauli iliyotolewa na mshambuliaji wa Paris Saint-Germain kuhusu nchi hiyo Jumapili iliyopita. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 aliondoka uwanjani akiwa amekasirika baada ya kuchapwa mabao 3-2 na Bordeaux katika mchezo wa ligi na kunaswa na kamera za uwanjani akiitaja nchi hiyo kama takataka. Ibrahimovic aliomba radhi kwa kauli yake hiyo lakini Valls ameonyesha kutofurahishwa na kumtaka mchezaji huyo kuchunga kauli zake kabla ya kuzungumza siku zijazo. Valls amesema alishangazwa na kauli hiyo kwani anadhani wachezaji soka wanapaswa kuonyesha mfano mbele ya jamii inayowazunguka na sio kutoka maneno ya hovyo ambayo yanaweza kuzusha hasira. Shirikisho la Soka la Ufaransa-FFF linafanyia uchunguzi tukio hilo na kama wakimkuta na hatia Ibrahimovic anaweza kulimwa adhabu.

No comments:

Post a Comment