Wednesday, April 1, 2015

ALABA HATIHATI KUIVAA DORTMUND.

BEKI wa kushoto wa Bayern Munich, David Alaba anatarajiwa kuukosa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Borussia Dortmund baada ya kupata majeruhi ya goti katika mchezo ambao Austria ilitoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Bosnia-Herzegovina Jana. Alaba ambaye ameshakaa nje kwa miezi mitatu kutokana na majeruhi kama hayo ya goti aliyopata Novemba mwaka jana, alikwua natarajiwa kufanyiwa vipimo zaidi leo jijini Munich. Beki huyo alitolewa nje baada ya kuumia muda mfupi kabla ya mapumziko huku akionekana kuchechemea kwa maumivu wakati akipelekwa nje. Bayern ambao wanaongoza La Liga na kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Ujerumani, wanatarajiwa kuchuana na FC Porto katika mchezo war obo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baadae mwezi huu.

No comments:

Post a Comment