BEKI mahiri wa klabu ya Borussia Dortmund Mats Hummels ameishushua Manchester United akidai kuwa hajawaahidi kujiunga nao katika majira ya kiangazi. United wamekuwa na mategemeo ya kutumia udhaifu wa Dortmund msimu huu wakiamini kuwa wanaweza kumnasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 26. Kumekuwa na taarifa kuwa Hummels aliwahi kumuahidi meneja wa zamani wa United Sir Alex Ferguson kwamba atakuja kuitumikia timu hiyo na kuwa tayari mpango huo ulikuwa umekamilika. Hata hivyo, Hummels amekanusha vikali taarifa hizo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akidai kuwa sio za kweli kama zinavyodaiwa. Pamoja na kutolewa nje inaaminika United bado itatuma ofa Dortmund kwa ajili ya kumsajili beki huyo kiangazi ili waweze kuimarisha safu yao ya ulinzi.

No comments:
Post a Comment