Thursday, April 2, 2015

HARRY KANE AITAMANI MICHUANO YA ULAYA YA VIJANA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amesema Harry Kane anataka kumaliza kazi katika michuano ya Ulaya kwa vijana chini ya umri wa miaka 21 itakayofanyika majira ya kiangazi mwaka huu. Mshambuliaji huyo wa Tottenham Hotspurs aliiifungia bao timu ya wakubwa ya Uingereza katika sekunde ya 79 toka aingie katika mchezo dhidi ya Lithuania Ijumaa iliyopita huku akipata namba katika kikosi cha kwanza katika mchezo uliofuata ambao walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Italia juzi. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha vijana chini ya miaka 21 cha nchi hiyo ambacho kilifuzu michuano hiyo bila kufungwa. Hodgson amesema Kane anataka kwenda na kikosi hicho kumaliza kazi ambayo tayari walikuwa wameianza vyema.

No comments:

Post a Comment