KOCHA wa timu ya taifa ya Iran, Carlos Queiroz amejiuzulu wadhifa wake huo baada ya kuinoa timu hiyo kwa miaka minne. Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid alichukua mikoba ya kuinoa Iran Aprili mwaka 2011 na kuliongoza taifa hilo kiislamu kushiriki michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka jana. Iran pia ilifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Asia nchini Australia mapema mwaka huu ambapo walikuja kufungwa na Iraq kwa changamoto ya mikwaju ya penati. Queiroz ambaye pia alikuwa kuwa msaidizi wa Sir Alex Ferguson kwa kipindi kirefu Manchester United alikuwa amesaini mkataba mpya Septemba mwaka jana ambao ungemfanya kuendelea kuinoa timu hiyo mpaka baada ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018.

No comments:
Post a Comment