Thursday, April 2, 2015

STERLING ADAI YEYE HAJALI SANA FEDHA.

MSHAMBULIAJI nyota wa Liverpool, Raheem Sterling amedai kuwa pesa sio vitu anavyovihusudu sana baada ya kuthibitisha kukataa ofa ya mkataba mpya ambao ungemuwezeza kulipwa kitita cha paundi 100,000 kwa wiki. Nyota huyo pia amesema hatazungumzia suala la mkataba mpya na klabu yake hiyo mpaka wakati wa majira ya kiangazi, bila kujali ofa gani kubwa atakayopewa katikati ya kipindi hicho. Sterling amesema hayuko kwa ajili ya pesa kwani yeye anataka kuzungumzia kuhusu kushinda mataji katika kipindi chote akiwa mchezaji. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza aliendelea kudai kuwa hataki kuzungumzia ni magari mangapi ataendesha au nyumbani ngapi atanunua kwani anataka kujitahidi kuwa bora kadri atakavyoweza. Sterling alijiunga na Liverpool akitokea Queens Park Rangers mwaka 2010, na hakuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza mpaka msimu uliofuatia.

No comments:

Post a Comment