RAIS wa klabu ya Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amedai kuwa rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter yuko tayari kubadilika kuliko inavyodhaniwa na wapinzani wake. Rummenigge ambaye ni mwakilishi wa umoja vilabu barani Ulaya-ECA amesema anadhani kuwa Blatter ameshutumiwa vya kutosha. Kutokana na shutuma hizo ambazo nyingie zikiwa za ufisadi, Rummenigge anaamini shirikisho hilo litabadilika kwa njia nzuri. Blatter mwenye umri wa miaka 79, anatarajia kugombea muhula mwingine wa tano katika uchaguzi wa shirikisho hilo utakaofanyika Mei 29 mwaka huu. Rais huyo anapewa nafasi kubwa ya kuwazidi wapinzani wake akiwemo Louis Figo kutoka Ureno, Michael Van Praag wa Uholanzi na Prince Ali wa Jordan.

No comments:
Post a Comment