Wednesday, April 1, 2015

DHARAU ZAIPONZA URENO.

TIMU ya taifa ya Ureno ikiwa bila nahodha wake Cristiano Ronaldo jana ilijikuta ikipokea kipigo cha kushtusha nyumbani cha mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa dhidi ya Visiwa vya Cape Verde. Ureno wanaongoza katika kundi lao la kufuzu michuano ya Ulaya mwakani lakini walimpumzisha Ronaldo katika mchezo huo dhidi ya Cape Verde ambao wapo nafasi ya 38 katika viwango vya ubora duniani. Mpaka mapumziko wageni hao kutoka bara la Afrika walikuwa mbele kwa mabao mwili ambayo yalifungwa na Odair Fortes na Admilson Gege. Wenyeji Ureno pia walimpoteza beki wao Andre Pinto aliyepewa kadi nyekundu katika dakika ya 60 ya mchezo huo.

No comments:

Post a Comment