Wednesday, April 1, 2015

MOURINHO AM-BEEP WENGER KWA WALCOTT.

KLABU ya Chelsea inafuatilia kwa karibu mwenendo wa suala la mkataba wa Theo Walcott na wanaweza kujitosa kumsajili kama ikiwezekana katika majira ya kiangazi. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza amekuwa katika mvutano na Arsenal juu ya mkataba mpya huku meneja Arsene Wenger akibanisha kuwa bado anataka kuendelea kuwa na winga huyo. Walcott mwenye umri wa miaka 25 hivi sasa anamalizia miezi 12 ya mwisho katika mkataba wake aliosaini miaka mitatu iliyopita. Pamoja na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Wenger bado Arsenal wanaonekana kuwa na nia ya kuendelea kuwa naye.

No comments:

Post a Comment