SHIRIKISHO la Soka la Uganda-FUFA limethibitisha leo asubuhi kumpatia kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Micho Sredojevic nyongeza ya mkataba wa miaka mitatu ambayo itamfanya kuendelea kuinoa timu hiyo mpaka mwaka 2018. Rais wa FUFA, Moses Magogo alibanisha taarifa hizo katika mkutano wa kila wiki wanahabari huko Mengo huku Micho mwenyewe akiwepo. Magogo amesema wamefikia hatua hiyo kwasababu kocha huyo amewawezesha kuwapa matokeo ya heshima katika michezo mikubwa na hakuna kocha yeyote aliyewahi kufanya hivyo huko nyuma. Rais huyo aliendelea kudai kuwa uongozi wake unaamini kuwa Micho anaweza kuwapeleka kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika 2017 baada ya kuikosa kwa hatua chache mwaka uliopita. Mara ya mwisho Uganda kushiriki michuano hiyo ilikuwa mwaka 1978.

No comments:
Post a Comment