Wednesday, April 1, 2015

TUNISIA WAUFYATA MBELE YA CAF.

HATIMAYE Shirikisho la Soka la Tunisia-TFF limesalimu amri mbele ya Shirikisho la Soka la Afrika-CAF kwa kuomba rdhi kama walivyoamriwa na kuepuka kufungiwa kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2017. Tunisia walikuwa wakitoa tuhuma juu penati yenye utata katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika ambao walichapwa na wenyeji Guinea ya Ikweta Januari 31 mwaka huu. Hata hivyo CAF ilitupilia mbali rufani ya Tunisia waliyokata dhidi ya faini ya dola 50,000 waliyotozwa kufuatia vurugu zilizofanywa na wachezaji wake. Wachezaji wa nchi hiyo wenye hasira walijaribu kumvamia mwamuzi baada ya mchezo huo Rajindraparsad Seechurn ambaye aliwazawadia wenyeji penati katika dakika za lala salama an kuwafanya kuupeleka mchezo katika dakika za nyongeza na kushinda kwa mabao 2-1. Tunisia ilikuwa inalituhumu shirikisho hilo kwa kupanga matokeo kutokana na maamuzi ya mwamuzi huyo lakini jambo hilo lilikanushwa vikali na viongozi wa CAF waliodai kuombwa radhi. CAF ilitishia kuwa kama Tunisia wasingeomba radhi kwa barua rasmi mpaka ifikapo Machi 31 wangeenguliwa katika mechi za kufuzu michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment