RAIS wa Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA, Sepp Blatter ametaka adhabu kali kuchukuliwa kwa timu au chama chochote kitakachokutwa na hatia ya kufanya mambo ya kibaguzi. Blatter raia wa Uswisi mwenye umri wa miaka 79 anafikiri adhabu zilizopo sasa zinaonyesha kutofanya kazi ipasavyo. Rais huyo amesema sasa hivyo wanapaswa kutumia sheria kama kuzisimamisha timu, kuwanyang’anya alama au hata kuwashusha daraja kama masuala ya kibaguzi yataendelea. Blatter ambaye anagombea tena nafasi ya urais wa FIFA Mei mwaka huu, alizungumza hayo katika mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF uliofanyika jijini Cairo, Misri jana.
No comments:
Post a Comment