KLABU ya Wigan Athletic imemtimua meneja wake Malky Mackay kufuatia kipigo cha mabao 2-0 walichopata nyumbani kutoka kwa Derby County jana. Wigan ambao walinyakuwa Kombe la FA na kushushwa daraja kutoka katika Ligi Kuu mwaka 2013 wako juu ya eneo la hatari ya kushuka daraja kwa tofauti ya alama tano huku kukiwa kumebaki michezo mitano. Mackay mwenye umri wa miaka 43, ambaye amewahi kuzinoa Watford na Cardiff City alichukua mikoba ya Wigan Novemba mwaka jana lakini amefanikiwa kuambulia alama 19 kati ya 72 na kuifanya timu hiyo kuwa katika hatari kushushwa daraja tena. Mwenyekiti wa Wigan David Sharpe aliuambia mtandao wa kabu hiyo kuwa uamuzi waliochukua ni mgumu lakini wanadhani yalihitajika kwa manufaa ya baadae.
No comments:
Post a Comment