SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF linatarajia kuteua mwenyeji mpya wa michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2017 kesho. Mwenyeji halisi Libya, alijitoa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mwaka jana kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea hivi sasa. Kamati ya utendaji ya CAF katika mkutano wake mkuu jijini Cairo inatarajiwa kuteua mwenyeji mpya kati ya nchi za Algeria, Gabon na Ghana. CAF pia inatarajiwa kutoa ratiba ya mechi za kufuzu michuano hiyo ambayo itazijumuisha timu za Morocco na Tunisia hiyohiyo kesho. Morocco walikuwa wamefungiwa kushiriki fainali mbili za michuano hiyo kwa kushindwa kuandaa michuano iliyofanyika mapema mwaka huu lakini adhabu hiyo ilitenguliwa baada ya kushinda rufani yao katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS. Tunisia wao waliepuka adhabu ya kufungiwa baada ya kuomba radhi CAF kwa kulituhumu shirikisho hilo kwa upendeleo.
No comments:
Post a Comment