POLISI nchini Uturuki inawashikilia watu wakihusishwa na mtu aliyeshambulia basi la timu ya Fenerbahce mwishoni mwa wiki iliyopita. Basi la timu hiyo lilishambuliwa kwa risasi na mtu mwenye silaha wakati wakirejea nyumbani baada ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Rizerspor Jumamosi iliyopita na kumuumiza dereva wake huku wachezaji na viongozi wote wakitoka salama. Dereva huyo alikimbizwa hospitalini kutokana na majeruhi hayo na madaktari wamethibitisha kukuta kitu mfano wa chuma kichwani mwake. Gavana wa mji wa Trabzon Abdul Cecil Oz sasa amethibitisha kukamatwa kwa watu hao wawili katika eneo la Surmene wakihusishwa na tukio hilo. Kufuatia tukio hilo Shirikisho la Soka la Uturuki limesimamisha Ligi Kuu ya nchi hiyo ili kusubiri matokeo ya uchunguzi.

No comments:
Post a Comment